

Lugha Nyingine
Maofisa wa AU na UN watoa wito wa vitendo halisi kukabiliana na jangwa na ardhi kukosa rutuba barani Afrika
Maofisa na wataalamu wa Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa (UN) wametoa wito wa hatua za haraka kuchukuliwa ili kukabiliana na tishio la jangwa linaloongezeka na ardhi kukosa rutuba barani Afrika.
Wito huo umetolewa katika mkutano wa wataalamu uliojadili kwa kina Pendekezo la Ukuta wa Kijani la Umoja wa Afrika, uliofanyika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.
Akizungumza kwenye mkutano huo, mkurugenzi mkuu wa Muungano wa Haki ya Mabadiliko ya Tabianchi Afrika Mithika Mwenda amesema, serikali za nchi za Afrika zinatakiwa kuchukua hatua za haraka kuokoa bara hilo kutoka hatari kubwa ya jangwa, inayotokana na mabadiliko ya tabianchi, matumizi yasiyo endelevu ya maliasili, na uharibifu wa mfumo wa ikolojia ya misitu.
Ameonya kuwa, Jangwa la Sahara linaendelea kuelekea kusini huku Jangwa la Kalahari likielekea kaskazini, na kuwa ishara ya wazi ya haja ya kupunguza utoaji mkubwa wa hewa chafu.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma