Kenya yazindua jukwaa la wingu kuboresha usambazaji wa chanjo

(CRI Online) Mei 15, 2025

Wizara ya Afya nchini Kenya imezindua jukwaa la wingu ili kuhakikisha kuwa chanjo zinawasilishwa katika maeneo ya nchi hiyo bila ya usumbufu.

Waziri wa Wizara hiyo Aden Duale amesema, Mlango wa Kitaifa wa Kielektroniki wa Chanjo na Kinga utaanzisha hazina ya wakati halisi ya usimamizi wa takwimu za chanjo na kinga. Amesema jukwaa hilo la kidijitali litaboresha utoaji maamuzi na kuongeza uwazi, ufuatiliaji, uwajibikaji, na ufanisi katika huduma ya usambazaji wa chanjo nchini humo.

Amesema mlango huo unalenga kuimarisha miundombinu ya kinga nchini Kenya huku ukilinda afya ya watoto na watu wa makundi mengine yaliyo hatarini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha