

Lugha Nyingine
Kijiji cha mfano cha kilimo kinachofadhiliwa na China chazinduliwa nchini Zimbabwe
Kijiji cha mfano cha kilimo kinachofadhiliwa na China kimezinduliwa rasmi jana jumatano katika Wilaya ya Shamva, mkoa wa Mashonaland ya Kati nchini Zimbabwe, kwa lengo la kuboresha uzalishaji wa kilimo kwa wakulima wa vijijini.
Kijiji hicho, ambacho ni cha pili cha aina yake kuanzishwa na kundi la wataalamu wa kilimo wa China nchini Zimbabwe, kinachukua uzoefu wa China katika kuondokana na umasikini, na pia kinalenga kuwasaidia wakulima wa huko kubadilika kutoka kilimo cha kujikimu na kuwa na mtazamo wa kilimo cha kibiashara.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Naibu Waziri wa Ardhi, Kilimo, Uvuvi, Maji na Maendeleo Vijijini wa nchini Zimbabwe, Vangelis Haritatos amesema, kijiji hicho kinaonyesha mtazamo wa pamoja kwa ajili ya mageuzi ya kilimo kati ya nchi hiyo na China.
Naye Balozi wa China nchini Zimbabwe Zhou Ding ambaye pia alishiriki kwenye hafla ya uzinduzi huo, amesema mpango huo unaendana na safari ya China ya maendeleo na kuondokana na umasikini.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma