Rais wa China atuma salamu za pongezi rais mpya wa Togo

(CRI Online) Mei 16, 2025

Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa Jean-Lucien Savi de Tove kwa kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Togo.

Katika salamu hizo, rais Xi amesema, katika Mkutano wa mwaka 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika mjini Beijing, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeimarishwa kuwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote, hatua ambayo imefungua ukurasa mpya wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Rais Xi amesisitiza kuwa anaweka mkazo mkubwa katika maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili, na anapenda kushirikiana na viongozi wa Togo, kutumia fursa ya kutekeleza matokeo yaliyofikiwa katika Mkutano wa FOCAC wa Beijing, kuenzi urafiki wa jadi, kupanua ushirikiano katika sekta mbalimbali, ili kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha