Safari ya Utafiti wa “China Inayosonga Mbele” 2025 ya People’s Daily Online yaanza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 16, 2025

Safari ya utafiti wa “China Inayosonga Mbele” mwaka 2025 ya waandishi wa habari wa People’s Daily Online yameanza rasmi huko Shenyang, Mkoa wa Liaoning na Hefei, Mkoa wa Anhui.

Mwaka 2025 ni mwaka wa mwisho wa utekelezaji wa “Mpango wa 14 wa Maendeleo ya Miaka Mitano (2021-2025) ”, timu 31 za utafiti za People’s Daily Online zimekwenda kwa mfululizo sehemu mbalimbali nchini China, zikilenga kufanya mahojiano na kukusanya habari kufuatia wazo jipya la maendeleo juu ya " uvumbuzi, uratibu, hali ya kijani ya mazingira, uwazi na ujumuishi".

Ujumbe wa waandishi wa habari wa Utafiti wa “China Inayosonga Mbele” 2025 wa People’s Daily Online ukiingia katika Mji wa Shenyang, Mkoa wa Liaoning kufanya mahojiano na kukusanya habari.(Mpiga picha: Zhou Songxue/People’s Daily Online)

Ujumbe wa waandishi wa habari wa Utafiti wa “China Inayosonga Mbele” 2025 wa People’s Daily Online ukiingia katika Mji wa Hefei, Mkoa wa Anhui kufanya mahojiano na kukusanya habari.(Mpiga picha: Miao Zijian/People’s Daily Online)

Safari ya Utafiti wa“China Inayosonga Mbele” 2025 ya waandishi wa habari wa People’s Daily Online ikichukua mada ya "Maendeleo ya Ubora wa Juu katika Miaka Mitano " inalenga kusimulia hadithi za China kuhusu maendeleo ya uchumi yanayotegemea uvumbuzi na mageuzi ya kina kwa pande zote. Safari hiyo imeanza mwezi Mei na itaendelea hadi mwisho wa mwaka huu. Timu mbalimbali za utafiti za waandishi wa habari zitatumia vya kutosha njia za vyombo mbalibmali vya habari, na kutumia vilivyo nguvu bora ya lugha za makabila mbalimbali ya China na lugha 18 za kigeni, ili kuonyesha ipasavyo mafanikio ya maendeleo ya miaka mitano katika sehemu mbalimbali nchini China, na kuhamasisha ari ya watu ya kufanya juhudi kwa mshikamano na kusonga mbele kwa pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha