

Lugha Nyingine
Maonesho ya Biashara ya Huduma ya Kimataifa ya China kufanyika Septemba
Septemba 12, 2024, Maonesho ya Biashara ya Huduma ya Kimataifa ya China (CIFTIS) 2024 yalifanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha Beijing. (Zhou Guangping/Xinhua)
Maonesho ya Biashara ya Huduma ya Kimataifa ya China (CIFTIS) 2025 yatafunguliwa tarehe 10, Septemba mjini Beijing, ambapo Australia itakuwa nchi mgeni mheshimiwa.
Ofisa wa Idara ya Biashara ya Beijing Zhao Qizhou Alhamisi kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, kuanzia mwaka huu, maonesho hayo yatafanyika kila ifikapo Jumatano ya pili ya mwezi Septemba.
Maonesho hayo yatafanyika kwenye eneo la Bustani ya Shougang, ambayo ni mabaki ya viwanda yenye ukubwa wa kilomita 3 za mraba , na pia ilikuwa ni sehemu ya kufanyika kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022.
Maonesho hayo yatahusisha sekta za fedha, utamaduni na utalii, elimu, michezo, minyororo ya utoaji bidhaa , huduma ya afya na kadhalika.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma