

Lugha Nyingine
Meli kubwa zaidi ya kusafirisha magari yenye nafasi 9500 yafunga safari ya kwanza kwenda Ulaya kutoka Shanghai
Picha iliyopigwa tarehe 15, Mei ikionesha hafla ya kuipa jina meli ya Anji Ansheng iliyofanyika kwenye gati la magari la kimataifa la Shanghai Haitong. (Fang Zhe/Xinhua)
Meli kubwa ya kupita kiasi ya kusafirisha magari ya ro-ro (roll-on/roll-off) yenye nafasi 9,500 ya Anji Ansheng, ambayo iliundwa na China yenyewe, imefunga safari yake ya kwanza ya kwenda Ulaya kutoka Shanghai usiku wa jana tarehe 15, ikibeba magari 7,000 yaliyoundwa nchini China.
Meli hiyo ya Anji Ansheng iliundwa kwa uwekezaji wa Kampuni ya Usafirishaji ya SAIC Anji, ikitumia teknolojia ya mstari wa mbele zaidi kutoka usanifu hadi uundaji. Urefu wa jumla wa meli hiyo umefikia mita 228, na upana wake ni mita 37.8, ukiwa meli kubwa ya kisasa ya ro-ro ya kusafirisha magari yenye utoaji chache wa kaboni, ambayo ni meli ya kutumia teknolojia ya kisasa kwa kubeba magari mengi zaidi duniani.
Katika mwisho wa mwezi Aprili, meli ya kusafirisha magari ya umeme yenye nafasi 9,200 sanifu ya kampuni ya BYD “Shenzhen” ilifunga safari yake ya kwanza, ikiweka rekodi mpya ya meli inayoweza kubeba magari mengi zaidi duniani. Sasa safari ya kwanza ya meli ya Anji Ansheng imevunja tena rekodi hiyo.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma