

Lugha Nyingine
Kijiji cha Kielelezo cha Kilimo kilichoanzishwa kwa msaada wa China nchini Zimbabwe chazinduliwa
Tarehe 14, Mei, 2025, mtaalamu wa kilimo akieleza kuhusu uzalishaji wa kilimo kwa mwanakijiji mwenyeji kwenye kijiji cha kielelezo cha kilimo kilichoanzishwa kwa msaada wa China katika Wilaya ya Shamva, Mkoa wa Mashonaland ya Kati nchini Zimbabwe. (Xinhua/Tafara Mugwara)
Kijiji cha kielelezo cha kilimo kilichoanzishwa kwa msaada wa China kilizinduliwa rasmi tarehe 14 mwezi huu katika Wilaya ya Shamva, Mkoa wa Mashonaland ya Kati nchini Zimbabwe. Kijiji hicho kinalenga kuinua ufanisi wa uzalishaji wa kilimo wa vijiji vya Zimbabwe.
Kijiji hicho cha kielelezo ni kijiji cha pili cha aina hii kilichoanzishwa na wataalamu wa kilimo kutoka China, kikitumia uzoefu wa China wa kupunguza umaskini kwa kuwasaidia wakulima wa huko kubadilisha hali ya kilimo cha kujitosheleza tu hadi kuendeleza kilimo cha kibiashara.
Kikundi cha wataalamu walisema, makumi ya familia wamepata uzoefu wa kilimo endelevu kwa kupitia mfumo wa umwagiliaji wa kisasa, mbegu za aina ya kuzalisha mazao mengi na kukinga ukame, teknolojia ya kilimo bora cha kuongeza uzalishaji, na mfumo wa mifugo ya jumla.
Naibu Waziri wa Ardhi, Kilimo, Uvuvi, Maji na Maendeleo ya Kijiji Vangelis Haritatos kwenye hafla ya uzinduzi waliyoshiriki maofisa wa China na Zimbabwe na wanakijiji wenyeji alisema, kijiji hicho cha kielelezo kimeonesha matarajio ya pamoja ya nchi mbili ya kubadilisha muundo wa kilimo.
Alisema, “Mradi huo umeonesha urafiki wa muda mrefu na uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya Zimbabwe na China, ambao umekita mizizi kwenye kuheshimiana, kustawi kwa pamoja na matarajio ya pamoja juu ya maendeleo endelevu.” Aliongeza kuwa, kuongeza uwezo wa wakulima ni muhimu sana kwa ustawishaji wa vijiji na kuhakikisha jamii inapata maendeleo kwenye mabadiliko ya tabianchi.
Tarehe 14, Mei, 2025, mtaalamu wa kilimo akieleza kuhusu uzalishaji wa kilimo kwa mwanakijiji mwenyeji kwenye kijiji cha kielelezo cha kilimo kilichoanzishwa kwa msaada wa China katika Wilaya ya Shamva, Mkoa wa Mashonaland ya Kati nchini Zimbabwe. (Xinhua/Tafara Mugwara)
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma