

Lugha Nyingine
Msomi wa Côte d'Ivoire alaani Serikali ya Marekani kwa kutumia tishio la ushuru kwa mahusiano
Mwanauchumi na mtaalamu wa masuala ya maendeleo kutoka Côte d'Ivoire, Alexis Bih, amesema sera ya Marekani ya kutumia tishio la ushuru kiholela inaonyesha kupuuza haki za kiuchumi za nchi zinazoendelea na kuanzisha mifano mitatu hatari katika biashara ya kimataifa.
Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China Xinhua, Bw. Bih ametaja maeneo hayo matatu kuwa ni kutumiwa kiholela kwa kisingizio cha "usalama wa nchi" katika biashara ya bidhaa za kilimo, kuweka vikwazo vikali zaidi ya viwango vya Shirika la Biashara la Dunia (WTO) kwa nchi zinazoendelea ambazo zinafuata sheria za biashara, na mwisho ni kuharibu kwa makusudi fursa za maendeleo zinazopata nchi za Dunia ya Kusini kupitia makubaliano ya kikanda ya biashara.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma