

Lugha Nyingine
Vyombo vya habari vya Ethiopia na China vyaahidi uhusiano wa karibu ili kuimarisha mawasiliano ya kitamaduni
Vyombo vya habari vya Ethiopia na China vimeeleza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kina ili kuboresha maelewano ya pamoja na kuimarisha mawasiliano ya kiutamaduni.
Kauli hiyo imetolewa wakati wa jukwaa la ngazi ya juu lililofanyika jumatano wiki hii mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, chini ya kaulimbiu “Kuitazama China: Kuboresha Ushirikiano wa Vyombo vya Habari vya China na Ethiopia.”
Mkutano huo ulioandaliwa kwa pamoja na Idara kuu ya Radio na Televisheni ya China, Idara ya Huduma za Mawasiliano ya Serikali ya Ethiopia, na Ubalozi wa China nchini Ethiopia, ulikutanisha washiriki 200, wakiwemo maofisa waandamizi wa Ethiopia, wanadiplomasia wa China, wajumbe wa vyombo vya habari kutoka nchi zote mbili, wasomi, na watunga maudhui wa Afrika.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma