Kampuni ya Huawei yazindua njia ya kisasa ya umeme wa jua kuongeza kasi ya mageuzi ya kijani barani Afrika

(CRI Online) Mei 16, 2025

Kampuni ya teknolojia ya mawasiliano ya China, Huawei, itatumia njia ya kisasa ya umeme wa jua kusaidia mageuzi ya kijani barani Afrika.

Akizungumza jijini Nairobi, Kenya, wakati wa uzinduzi wa Bidhaa ya Uvumbuzi wa Viwanda na Biashara ya FusionSolar Eastern Africa ya kampuni ya Huawei, Mkurugenzi Mkuu wa Nishati ya Kidijitali wa kampuni hiyo kanda ya Afrika Mashariki, Du Peng, amesema uchumi wa kijani kwa bara la Afrika unaweza kutimizwa kama viwanda na serikali zitashirikiana kwa pamoja kuboresha matumizi ya nishati safi, ikiwemo umeme wa jua.

Bidhaa hiyo ambayo ni betri ya kisasa, tayari imetambulishwa katika maeneo mengine ya bara la Afrika.

Du amesema, matumizi ya teknolojia mpya za umeme wa jua katika masoko ya bara la Afrika yatakuwa ni muhimu sana katika kutimiza uchumi wa kijani na nyumbufu katika bara hilo ambalo tayari linakabiliwa na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha