

Lugha Nyingine
Kampuni ya kuunda magari ya China yazindua magari yake yanayotumia umeme katika soko la Ethiopia
Kundi la Kampuni za GAC, ambalo ni muundaji magari kutoka mkoa wa Guangdong nchini China, limezindua aina mbili za magari yake yenye kutumia nishati ya umeme nchini Ethiopia, ikiwa ni mara ya kwanza kwa magari ya kundi hilo kuingia kwenye soko la Ethiopia.
Kundi hilo limezindua magari yake aina ya AION Y na ES9 katika hafla iliyofanyika Jumamosi mjini Addis Ababa.
Akiongea katika hafla hiyo, kamishna wa Kamisheni ya Uwekezaji ya Ethiopia, Zeleke Temesgen, amesema serikali ya nchi hiyo imechukua hatua madhubuti kuhamasisha matumizi ya magari yanayotumia umeme ili kuharakisha mpito wa nchi hiyo kuelekea usafiri wa kutumia umeme.
Kamishna huyo ametoa wito kwa kundi la GAC kujenga kiwanda cha kuunda magari nchini Ethiopia ili kutumia vizuri uwekezaji nafuu na fursa kubwa za soko nchini humo, na kuharakisha juhudi za Ethiopia kuelekea usafiri unaotumia nishati safi.
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma