

Lugha Nyingine
Mashambulizi ya wanamgambo yasababisha vifo vya watu 14 magharibi mwa Sudan
Takriban raia 14 wameuawa wakati wanamgambo wa Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) walipofanya mashambulizi ya mizinga huko El Fasher, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kaskazini, magharibi mwa Sudan.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamati ya uratibu wa mapigano ya Sudan, mashambulizi hayo yalilenga Soko la Naivasha lililopo kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao ya AbuShouk, pamoja na vitongoji kadhaa vya kaskazini mwa mji wa El Fasher.
Asasi ya Chumba cha Dharura ya Kambi ya Abu Shouk pia imethibitisha kwenye taarifa yake kuwa watu 14 waliuawa katika shambulio hilo.
Kundi la mtandao wa madaktari wa Sudan pia limesema mashambulizi yamesababisha hasara kubwa, na kutokana na hali mbaya ya usalama, bado hawajaweza kubaini idadi kamili ya waliouawa na kujeruhiwa.
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma