

Lugha Nyingine
Mwenyekiti kamisheni ya Umoja wa Afrika aeleza wasiwasi wake kuhusu mapigano ya hivi karibuni mjini Tripoli
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Bw. Mahmoud Ali Youssouf ameeleza "wasiwasi wake" juu ya mapigano makali yaliyotokea hivi karibuni katika mji wa Tripoli nchini Libya ambayo yamesababisha vifo na uharibifu wa mali, akisisitiza umuhimu wa kuondoa silaha mjini Tripoli.
Bw. Youssouf amekaribisha usimamishaji vita wa hivi karibuni na kurejea kwa hali ya utulivu, lakini amehimiza pande zote kujiepusha na vitendo au kauli zinazoweza kuyumbisha zaidi hali tete ya usalama.
Pia amesisitiza uungaji mkono wa Umoja wa Afrika kwa juhudi za kurejesha utulivu na kudumisha haki za kukusanyika na uhuru wa kutoa maoni.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa yenye makao yake mjini Tripoli (GNU) imesema hali ya utulivu imerejea mjini Tripoli, baada ya siku mbili za mapigano makali kati ya makundi hasimu, yaliyosababisha vifo vya takriban watu sita.
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma