Rais Xi asisitiza kukamilisha kwa sifa bora kazi ya kuandaa Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Miaka Mitano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 20, 2025

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amesisitiza kutoa maamuzi kwa njia ya kisayansi, kwa demokrasia na kwa mujibu wa sheria ili kuhakikisha mpango wa 15 wa China wa maendeleo ya miaka mitano ya uchumi na jamii unaandaliwa na kukamilika kwa sifa bora.

Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), amesema hayo katika maagizo yake ya hivi karibuni kuhusu kazi ya kufanya Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Miaka Mitano (2026-2030).

Rais Xi amesema kuwa kuandaa mpango wa maendeleo ya miaka mitano kwa njia ya kisayansi na kuutekeleza ni uzoefu muhimu wa Chama cha Kikomunisi cha China katika kufanya utawala wa nchi.

“Uandaaji na utekelezaji wa Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Miaka Mitano una umuhimu mkubwa kwa kutimiza kikamilifu mipango ya kimikakati iliyoamuliwa kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC na kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China,” Rais Xi amesema.

Amesisitiza umuhimu wa kuunganisha upangaji mpango wa hali ya juu, kutafuta mapendekezo kutoka kwa umma, kuimarisha utafiti na majadiliano, na kujenga mwafaka mpana.

Kuanzia mwaka 2026, China itaanza utekelezaji wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano ya maendeleo ya uchumi na jamii.

Hivi sasa, Kamati Kuu ya CPC iko katika kuandaa mswada wa mapendekezo ya mpango huu, na idara husika zinajipanga kukukusanya maoni na mapendekezo kutoka kwa maofisa, watu wa sekta mbalimbali, pamoja na wataalam na wasomi kwa kupitia njia mbalimbali katika siku za usoni.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha