Uchumi wa China waonyesha uhimilivu mkubwa licha ya shinikizo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 20, 2025

Picha iliyopigwa tarehe 25 Aprili 2025 ikionyesha meli ya mizigo ikiendeshwa katika Bandari ya Tianjin mjini Tianjin, kaskazini mwa China. (Xinhua/Zhao Zishuo)

Picha iliyopigwa tarehe 25 Aprili 2025 ikionyesha meli ya mizigo ikiendeshwa katika Bandari ya Tianjin mjini Tianjin, kaskazini mwa China. (Xinhua/Zhao Zishuo)

BEIJING - Uchumi wa China umehimili shinikizo na kuendelea kuongezeka kwa utulivu, ukiendelea kudumisha mwelekeo wa maendeleo mazuri huku kukiwa na changamoto za ndani na kuongezeka kwa mishtuko kutoka nje, Fu Linghui, Msemaji Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) amesema jana Jumatatu.

Fu amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba hali ya jumla ya wa uchumi wa China ya kuwa mzuri haujabadilika, na kwamba kuna mazingira kadhaa mazuri ya kuendelea kuimarika kwa uchumi.

Takwimu zilizotolewa na NBS zinaonyesha kuwa mauzo ya rejareja ya bidhaa za matumizi nchini China, ambayo ni kiwango muhimu cha nguvu ya matumizi ya nchi hiyo, yaliongezeka kwa asilimia 5.1 mwezi Aprili hadi kufikia yuan trilioni 3.72 (dola za Kimarekani kama bilioni 517.27) kuliko mwaka jana wakati kama huo.

Kuanzia Januari hadi Aprili, mauzo ya rejareja ya bidhaa za matumizi yaliongezeka kwa asilimia 4.7 kuliko kipindi hicho cha mwaka jana, kiasi ambacho kimeongezeka kutoka asilimia 4.6 katika miezi mitatu ya kwanza, kwa mujibu wa NBS.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa katika miezi minne ya kwanza, kiwango cha uzalishaji wa huduma kiliongezeka kwa asilimia 5.9, ikiwa ni asilimia 0.1 haraka kuliko ile ya robo ya kwanza.

Mwezi Aprili, jumla ya thamani ya bidhaa zilizoagizwa na kuuzwa nje ilifikia yuan trilioni 3.84, ongezeko la asilimia 5.6 kuliko mwaka jana wakati kama huo, takwimu hizo zimeonyesha. Na kwamba, kuanzia Januari hadi Aprili, thamani ya jumla ya uagizaji na uuzaji nje bidhaa ya China iliongezeka kwa asilimia 0.6, ikichukua asilimia 64 ya thamani ya jumla ya biashara ya nje.

Aidha, takwimu hizo zinaonyesha kuwa, katika kipindi cha miezi minne ya kwanza, kampuni binafsi zilishuhudia ongezeko la asilimia 6.8 la uagizaji na uuzaji nje bidhaa, likichukua asilimia 56.9 ya jumla ya biashara ya China, ambayo ni ongezeko la asilimia 2.3 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Pia takwimu hizo zinaonyesha kuwa, uwekezaji wa mali zisizohamishika wa China ulipanda kwa asilimia 4 mwaka hadi mwaka katika miezi minne ya kwanza ya 2025 hadi kufikia yuan trilioni 14.7. Na kwamba, Bila ya sekta ya nyumba, uwekezaji wa mali zisizohamishika nchini humo ulikua kwa asilimia 8katika kipindi hicho kuliko mwaka jana.

Katika kipindi hicho, uwekezaji wa miundombinu uliongezeka kwa asilimia 5.8, huku uwekezaji wa viwanda ukiongezeka kwa asilimia 8.8, takwimu zinaonyesha.

Hata hivyo, Fu amesema kuwa mazingira ya sasa ya kimataifa yanaendelea kuwa magumu na yenye changamoto, huku kuongezeka kwa hatua za upande mmoja na kujihami kukileta changamoto kubwa kwa utaratibu wa kimataifa wa uchumi na biashara na kuzuia ukuaji wa uchumi duniani.

"Lakini mwelekeo wa ushirikiano wa kimataifa wa kunufaishana hautabadilika, na dhamira ya China ya kupanua ufunguaji mlango itaendelea kuwa thabiti," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha