 
				 
			Lugha Nyingine
Msumbiji yapata tuzo kwa maendeleo katika udhibiti wa malaria
Ofisi ya Rais wa Msumbiji imetangaza kuwa Msumbiji imepata tuzo ya kupambana na ugonjwa wa malaria iliyotolewa kwenye mkutano wa 78 wa Baraza la Afya Duniani (WHA) unaofanyika mjini Geneva, ambapo waziri wa afya wa nchi hiyo Bw. Ussene Isse amepokea tuzo hiyo kwa niaba ya Msumbiji.
Tuzo hiyo imeonesha juhudi za Msumbiji katika kuzuia malaria, ikiwa ni pamoja na usambazaji wa vyandarua kwa watu wengi, kampeni za unyunyiziaji wa dawa ndani, kuboresha huduma za uchunguzi, na kuimarisha ufuatiliaji wa wagonjwa.
Maofisa wa serikali wamesema kuwa tuzo hiyo itaimarisha juhudi za Msumbiji za kutokomeza ugonjwa wa malaria na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, na inalenga kuhakikisha ugonjwa huo hauwi tishio tena kwa afya ya umma nchini Msumbiji na duniani.
 - Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China 
 - Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China 
 - UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika 
 - Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai 
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
