

Lugha Nyingine
Simulizi za Miji | Ruka, elea, na pata uhondo wa chakula kivyako kupitia Yueyang ya China, mji wa historia na ushairi
"Kwa mbali, ninachungulia maji na milima ya Ziwa Dongting yenye utando wa kijani; Kisiwa cha Junshan huonekana kama konokono wa jade aliyepumzika kwenye sahani ya madini ya fedha." - Liu Yuxi, "Kuchungulia Ziwa Dongting"
Je, unatamani kujaribu kupata mahaba ambayo yana historia ya maelfu ya miaka? Elekea Yueyang, inayopatikana katika Mkoa wa Hunan katikati mwa China. Mji uliojaa mashairi, historia, na nafsi, Yueyang umedumisha uhai katika kazi za wanafasihi mashuhuri kama Liu Yuxi, Du Fu, na Fan Zhongyan. Ni antholoji inayoishi, ikisubiri kufanyiwa utalii.
Panda juu ya Mnara Yueyang na chukua mwonekano wa mandhari ambayo yamehamasisha vizazi vya waandishi. Juu ya maji ya Ziwa Dongting, siku za nyuma na sasa zinapatana katika mandhari ya kuvutia na urithi wa simulizi. Kama eneo la dhabihu ya kizalendo ya mshairi mashuhuri Qu Yuan, pia ni mahali pa kuzaliwa kwa utamaduni wa mashua ya dragoni, na mahali sahihi pa kufurahia sikukuu na mashindano ya mbio za mashua za dragoni zinazofanyika ili kuisherehekea.
Lakini Yueyang hutoa zaidi ya mwangwi wa siku za nyuma. Randaranda kupita ardhi oevu iliyostawi kijani na kutana na milu mpole, au kulungu wa Père David. Simama kidogo karibu na Bandari ya Chenglingji kushuhudia mapigo ya moyo ya biashara ya kisasa katika pilika. Na andaa neva zako za ladha kwa maajabu ya upishi. Nyamachoma ya moshi ya Yueyang, samaki freshi waliovuliwa, na chakula cha wali chenye harufu nzuri vitamgeuza mgeni yeyote kuwa mlaji wa bidii nyingi.
Yueyang iko tayari kwa simulizi za zamani na mpya, ikikusubiria wewe uanze safari ambako jadi na usasa hutiririka pamoja kama maji ya Ziwa Dongting lenyewe.
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma