Shughuli ya kukusanya maoni mtandaoni kuhusu Kuandaa “Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Miaka Mitano”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 21, 2025

Hivi karibuni, rais Xi Jinping alitoa agizo muhimu kuhusu kazi ya kuandaa “Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Miaka Mitano”, akisisitiza kuwa, ni lazima kufanya maamuzi kwa njia ya kisayansi, kwa demokrasia na kwa mujibu wa sheria, ili kuhakikisha kazi inakamilika kwa sifa bora. Ili kutekeleza agizo hilo muhimu la rais, shughuli ya kukusanya maoni kuhusu kazi hiyo imeanza mtandaoni jana tarehe 20, Mei.

Habari zimesema, kutokana na shughuli hiyo, ukurasa maalumu umewekwa kwenye tovuti na APP za People’s Daily, Shirika la Habari la China Xinhua, Kituo Kikuu cha Redio na Televisheni cha China na jukwaa la kusomea la “Xuexiqiangguo”, na watu wanaweza kutoa maoni yao kwenye tovuti husika. Shughuli hiyo ya kukusanya maoni itafanyika kwa mwezi mmoja, na maoni husika yanayokusanywa yatapelekwa kwa Kamati Kuu ya Chama kujadiliwa wakati wa kutoa maamuzi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha