China yaitaka Marekani kuacha kuingiza siasa katika ufuatiliaji wa chanzo cha COVID-19

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 21, 2025

Kituo cha kupima COVID-19 kikionekana Times Square mjini New York, Marekani, Mei 17, 2022. (Xinhua/Wang Ying)

Kituo cha kupima COVID-19 kikionekana Times Square mjini New York, Marekani, Mei 17, 2022. (Xinhua/Wang Ying)

GENEVA - Msemaji wa Ujumbe wa China kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi, jana Jumanne akijibu maoni yasiyo na msingi yaliyotolewa na ujumbe wa Marekani kwenye Mkutano wa 78 unaoendelea wa Baraza la Afya Duniani (WHA) ameitaka Marekani kukomesha kuingiza kwake siasa katika kufuatilia chanzo cha COVID-19 na kuacha kutoa shinikizo kwa mashirika ya kimataifa.

Msemaji huyo amesema inashangaza kwamba Marekani -- nchi ambayo awali ilitangaza kujiondoa kutoka kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) - sasa bila msingi wowote inashambulia nchi ambazo zimeongeza uungaji mkono kwa shirika hilo.

"Marekani kiushahidi imepoteza ufahamu wake wa kimsingi wa mema na mabaya. China daima imekuwa ikitoa msaada usio na ubinafsi, badala ya kile kinachoitwa ushawishi usiofaa, kwa WHO," msemaji huyo amesema katika taarifa.

Picha iliyopigwa Januari 30, 2023 ikionyesha nembo za Shirika la Afya Duniani (WHO) kwenye makao makuu ya WHO mjini Geneva, Uswisi. (Xinhua/Lian Yi)

Picha iliyopigwa Januari 30, 2023 ikionyesha nembo za Shirika la Afya Duniani (WHO) kwenye makao makuu ya WHO mjini Geneva, Uswisi. (Xinhua/Lian Yi)

Msemaji huyo amesisitiza kuwa tangu kuzuka kwa janga la COVID-19, China imekuwa ikinufaisha taarifa na mlolongo wa vinasaba vya virusi hivyo na jumuiya ya kimataifa kwa wakati na kwamba pia imetoa vifaa tiba na msaada wa kifedha kwa WHO na nchi 153, ikiwemo Marekani.

"Hii inaonyesha dhamira ya China katika kulinda manufaa ya pamoja ya binadamu wote," ameongeza.

Amesema kuwa, China inaunga mkono ufuatiliaji chanzo wa kisayansi unaoongozwa na WHO na imealika timu za wataalam wa WHO kwenda nchini China mara kadhaa kwa utafiti wa pamoja na kwamba juhudi hizo zimesababisha hitimisho la kimamlaka la kisayansi kwamba kuvuja maabara kwa COVID-19 kutoka China "ni kusiko na uwezekano mkubwa," ikionyesha uwazi wa China juu ya suala hilo.

Msemaji huyo amesema kuwa baadhi ya nchi, katika kujaribu kuficha mwitikio wao mbaya wa janga hilo, zimeamua kuchafua wengine, akiongeza kuwa ulaghai kama huo wa kisiasa wa masuala ya janga ni aibu na hautafanikiwa.

Picha hii iliyopigwa Januari 19, 2023 ikionyesha chanjo dhidi ya COVID-19 zilizotolewa na China zikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Yangon mjini Yangon, Myanmar. (Ubalozi wa China nchini Myanmar/kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha