

Lugha Nyingine
Waziri wa mambo ya nje wa China kuhudhuria hafla ya kutia saini Mkataba wa Kuanzishwa kwa IOMed
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning amesema, waziri wa mambo ya nje wa China, Bw. Wang Yi atahudhuria hafla ya kutia saini Mkataba wa Kuanzishwa kwa Shirika la Kimataifa la Usuluhishi (IOMed) mjini Hong Kong, Mei 30.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana Jumanne, msemaji Mao amesema kuwa, mwaka 2022, China na karibu nchi 20 zenye misimamo inayofanana zilizindua kwa pamoja mpango wa kuanzisha IOMed.
Kupitia juhudi za pamoja, mazungumzo kuhusu Mkataba wa Kuanzishwa shirika hilo yamehitimishwa, na pande zote zimekubali kuweka makao yake makuu ya shirika hilo mjini Hong Kong.
Kwa mujibu maelezo, mataifa 60 kutoka Asia, Afrika, Amerika ya Kusini na Ulaya, na karibu mashirika 20 ya kimataifa, ukiwemo Umoja wa Mataifa (UN), watatuma wawakilishi wa ngazi za juu kwenye hafla hiyo.
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma