Sekta ya kahawa Uganda yatupia macho soko linalokua la China

(CRI Online) Mei 21, 2025

Ujumbe wa wawekezaji wa China unafanya ziara nchini Uganda kuanzisha uhusiano wa kibiashara na wakulima wa kahawa wa nchi hiyo, wakati mahitaji ya kahawa yakiendelea kuongezeka katika soko la China linalopanuka kwa kasi.

Baada ya kutembelea mashamba mbalimbali ya kahawa na vyama vya ushirika vya wakulima katika maeneo ya mashariki na magharibi mwa Uganda, ujumbe huo wa China pamoja na maofisa wa ubalozi wa China na serikali ya Uganda, walikutana jana Jumanne kujadili mikakati ya kuimarisha usafirishaji wa kahawa kwenda China.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda Bw. Vincent Bagiire, amesema ziara ya ujumbe huo kutoka China inaashiria hatua muhimu katika kuimarisha biashara ya kilimo na uwekezaji kati ya nchi hizi mbili.

Ameongeza kuwa lengo la ziara hiyo ni kuonyesha uwezo wa sekta ya kahawa ya Uganda kuvutia uwekezaji katika uongezaji thamani, na kuitangaza kahawa ya Uganda kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha