Serikali ya Somalia na mashirika ya kibinadamu waongeza misaada kwa waathirika wa mafuriko

(CRI Online) Mei 21, 2025

Serikali ya Somalia na washirika wa kibinadamu wameongeza msaada kwa maelfu ya watu walioathiriwa na mafuriko ya ghafla kote nchini humo.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu (OCHA) imesema serikali ya Somalia imeanzisha kamati inayoundwa na mawaziri, maofisa wa kikanda na Idara ya Menejimenti ya Maafa ya Somalia (SoDMA) ili kuongoza mwitikio wa kukabiliana na mafuriko.

OCHA imesema mashirika mengine ya hisani pia yanasambaza msaada kwa kaya elfu 4 katika Jimbo la Banadir, na kwa sasa yamezifikia familia elfu moja katika wilaya za Wadajir, Hodan na Waberi.

Kwa mujibu wa OCHA, mvua kubwa na mafuriko vimesababisha vifo vya watu 17 na kuathiri watu wasiopungua elfu 84 kote nchini Somalia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha