Uzuri wa Majira: Xiaoman

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 21, 2025

Hamjambo! Mimi ni Sisi, mpenda kusafiri! Leo ni Xiaoman, au Matumba ya Nafaka, kipindi cha pili cha majira ya joto katika Kalenda ya Kilimo ya China. Jiunge nami kwenda Mji wa Nanyang, Mkoa wa Henan, katikati mwa China, na jionee hali ya hewa moto moto ya majira ya joto katika "Ghala la nafaka Katikati mwa China."

Kipindi cha Xiaoman ni kipindi ambacho nafaka za majira ya joto katika kaskazini mwa China, kama vile ngano, zinaanza kukomaa lakini hazijaiva kabisa. Katika eneo la kusini mwa China, kipindi hiki huwa na mvua nyingi na mpunga wa mapema huanza kuvunwa na kuhifadhiwa kwenye ghala.

Katika kipindi hiki cha Xiaoman, halijoto na unyevunyevu zitaongezeka, jambo ambalo linawafanya watu wahisi hasira kidogo! Ili kuondoa hisia hizi, wengi wanafanya mazoezi yanayofaa wakati majira ya joto kama vile kutembea, kukimbia na kucheza Tai Chi.

Kipindi hiki cha Xiaoman katika kalenda ya kilimo ya China pia ni wakati muhimu kwa shughuli za hariri. Katika zama za kale, watu waliamini kwamba mungu wa nondo hariri angeweza kulinda dhidi ya magonjwa na majanga yanayoathiri nondo wa hariri. Ili kutoa shukrani, wazalishaji wa hariri walikuwa wakifanya matambiko ya kuheshimu mungu katika kipindi hiki. Hapo zamani za kale, bidhaa maridhawa za hariri zilikuwa zikiuzwa nje ya nchi kupitia Njia ya Hariri. Leo, hariri ya China inaendelea kuifikia dunia kupitia Treni ya mwendo kasi ya China na Ulaya na meli za kibiashara.

"Wakati ngano inapoanza kukomaa, nondo wa hariri hula kwenye majani mabichi ya mforsadi." Katika kipindi hiki cha Xiaoman kilichojaa tumaini wakati vitu vyote vinapokua kuelekea ukomavu, ninawatakia maisha yako yawe mazuri!

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha