Kufuata nyayo za Xi Jinping kutembelea makundi manne makubwa ya mapango nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 22, 2025

Mapango ya Longmen, Mkoani Henan, katikati mwa China, yenye historia ya zaidi ya miaka 1,500, ni Eneo la Urithi wa Dunia lililoorodheshwa kwenye orodha ya UNESCO lenye umuhimu mkubwa duniani.

Rais wa China Xi Jinping alikagua Mapango ya Longmen Mei 19, 2025. Alisisitiza umuhimu wa kuhifadhi, kurithi na kuendeleza hazina hizo za utamaduni wa China.

Mapango ya Longmen ni moja kati ya makundi manne makubwa zaidi ya mapango ya dini ya Kibuddha, sambamba na Mapango ya Mogao na Mapango ya Maijishan Mkoani Gansu, na Mapango ya Yungang Mkoani Shanxi.

Makundi hayo manne makubwa ya mapango ya China ni vito vinavyong'ara vya urithi wa China, kila moja likiwa na thamani kubwa ya kihistoria na ya kiutamaduni.

Ziara za Rais Xi katika maeneo hayo yote manne zimeonesha ufuatiliaji wake wa bila kuyumbayumba kwa uhifadhi na uendeleaji wa utamaduni wa China. Uongozi wake unatoa mwelekeo dhahiri kwa kuhifadhi mzizi wa utamaduni wa China na kuhakikisha urithi wa kila mara wa ustaarabu wa China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha