

Lugha Nyingine
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China, Afghanistan na Pakistan wafanya mkutano usio rasmi mjini Beijing
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Mohammad Ishaq Dar na Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan Amir Khan Muttaqi wakifanya mkutano usio rasmi mjini Beijing, mji mkuu wa China, Mei 21, 2025. (Xinhua/Wang Ye)
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Mohammad Ishaq Dar na Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan Amir Khan Muttaqi wamefanya mkutano usio rasmi mjini Beijing jana Jumatano ambapo Wang, ambaye pia mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, aliongoza mkutano huo.
Mawaziri hao wa mambo ya nje wamesifu matokeo ya mazungumzo ya pande tatu kati ya China, Afghanistan na Pakistan, na kushiriki katika majadiliano ya kina juu ya kutumia zaidi uwezo mkubwa wa kifursa wa mfumo huo wa pande tatu na kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana.
Akitoa majumuisho ya matokeo ya mkutano huo, Wang amesema mawaziri hao wa mambo ya nje wamekubaliana kuwa nchi hizo tatu zinapaswa kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa na kudumisha uhusiano wa kirafiki miongoni mwa majirani.
“China inaziunga mkono Afghanistan na Pakistan katika kufuata njia za maendeleo ambazo zinazofaa kwa hali zao za kitaifa na kutetea mamlaka, usalama na hadhi yao,” Wang amesema.
Amesema kuwa, mawaziri hao wamekubaliana kufanya Mazungumzo ya sita ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China-Afghanistan-Pakistan mjini Kabul mapema iwezekanavyo.
Kwa mujibu wake, Afghanistan na Pakistan zimeeleza nia ya kuinua uhusiano wa kidiplomasia wa pande mbili, huku pande zote mbili zikiwa zimekubaliana kimsingi kutuma mabalozi haraka.
“China inakaribisha hatua hii na inapenda kuendelea kuhimiza uboreshaji uhusiano kati ya Afghanistan na Pakistan,” Wang amesema.
Katika kuzidisha ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, mawaziri hao wamekubaliana kupanua Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan hadi Afghanistan na kuimarisha maendeleo ya miundombinu ya muunganisho wa kikanda.
“China na Pakistan zinaunga mkono ujenzi na maendeleo ya Afghanistan, na ziko tayari kuongeza biashara na Afghanistan ili kusaidia kuimarisha uwezo wake wa kujiendeleza,” amesema Wang.
Wang ameeleza kuwa, nchi hizo tatu zimekubaliana kupinga ugaidi wa aina zote, kufanya usimamizi wa utekelezaji sheria na ushirikiano wa kiusalama, kupambana na nguvu za kigaidi zinazofuatiliwa na kila upande, na kuendelea kuwa macho dhidi ya uingiliaji wa nje katika masuala ya ndani ya nchi za kikanda.
Mawaziri hao wa mambo ya nje wametoa wito wa juhudi za kulinda amani na utulivu wa kikanda ili kuweka mazingira mazuri ya nje yanayosaidia maendeleo ya nchi hizo tatu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Mohammad Ishaq Dar na Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Afghanistan Amir Khan Muttaqi wakifanya mkutano usio rasmi mjini Beijing, mji mkuu wa China, Mei 21, 2025. (Xinhua/Wang Ye)
Shughuli za kiutamaduni zafanyika kwenye Jukwaa la Russia na China mjini Khabarovsk, Russia
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma