

Lugha Nyingine
Rais Xi azihimiza China na Ufaransa kuwa nguvu za kutegemewa kwa kudumisha utaratibu wa kimataifa
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping jana Alhamisi alipozungumza na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa njia ya simu amezihimiza China na Ufaransa kuwa nguvu ya kutegemewa kwa kudumisha utaratibu wa kimataifa, kuwa nguvu ya ufunguaji mlango ya kuhimiza ongezeko la uchumi wa Dunia na kuwa nguvu ya kimaendeleo kwa kuongoza ushirikiano wa pande nyingi, akitoa wito kwa China na Ufaransa kulinda kwa pamoja mamlaka na heshima na hadhi ya Umoja wa Mataifa, kulinda sheria za biashara ya kimataifa na utaratibu wa uchumi wa dunia, na kutekeleza ushirikiano wa kweli wa pande nyingi.
Rais Xi amesema kuwa wakati wa ziara yake nchini Ufaransa mwezi Mei mwaka jana, pande hizo mbili zilikubaliana kufuata misingi ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Ufaransa ulio wa kujitawala na kujiamulia, kuwa na maelewano, kuwa na mtazamo wa kimkakati na kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja, na kuongeza mambo mapya chini ya muktadha wa nyakati za sasa na tangu hapo, maendeleo mapya mengi yamepatikana katika ushirikiano kati ya China na Ufaransa.
"Pande hizo mbili zinapaswa kuimarisha mawasiliano ya kimkakati na kujenga mwafaka mkubwa zaidi," Rais Xi amesema, akitoa wito wa kufanya juhudi za kutumia fursa kuzidisha ushirikiano katika maeneo ya jadi kama vile uwekezaji, usafiri wa ndege na anga ya juu, na nishati ya nyuklia, huku zikipanua ushirikiano katika sekta mpya za uchumi wa kidigitali, maendeleo ya kijani, matibabu ya kisayansi na teknolojia ya viumbe, na uchumi wa utunzaji wa wazee.
Pia amesisitiza kuimarisha mawasiliano ya kitamaduni na kuhimiza urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili.
Rais Xi amesisitiza kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 80 tangu kupatikana kwa ushindi wa Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti na kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa.
Rais Xi amesema, "China na Ufaransa zote ni nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi kubwa za kujitawala na kujiamulia, pia ni waanzilishi na wajenzi wa utaratibu wa kimataifa wa baada ya vita", nchi hizo mbili zinapaswa kuimarisha mshikamano na ushirikiano.
Amesema, Kadiri hali ya kimataifa inavyozidi kuwa na utatanishi, ndivyo China na Ufaransa zinavyohitaji kufanya chaguo sahihi la kimkakati.
Kwa upande wake, Macron amesema uhusiano kati ya Ufaransa na China na ule wa kati ya Umoja wa Ulaya na China ni wenye umuhimu sana na wenye maana kubwa duniani.
"Haijalishi namna gani hali ya kimataifa inavyobadilika, Ufaransa inaweka umuhimu mkubwa kwenye uhusiano wake na China, na msimamo wake juu ya kanuni ya kuwepo kwa China moja hautakuwa na mabadiliko yoyote," amesema.
Ikikabiliwa na hali ya kimataifa inayobadilika kwa haraka, rais huyo wa Ufaransa amesema nchi yake inapenda kuimarisha mawasiliano na uratibu na China juu ya masuala makubwa, kubeba wajibu wa nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuzuia kupamba moto na kuenea kwa migogoro ya kimaeneo, na kwa pamoja kulinda amani na utulivu wa kimataifa na wa kikanda.
Shughuli za kiutamaduni zafanyika kwenye Jukwaa la Russia na China mjini Khabarovsk, Russia
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma