

Lugha Nyingine
Kampuni zenye uwekezaji wa Marekani zakaribishwa kuzidisha ushirikiano wa kunufaishana na China
Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Jamie Dimon, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na ofisa mtendaji mkuu wa JPMorgan Chase, mjini Beijing, Mei 22, 2025. (Xinhua/Zhang Ling)
BEIJING - Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng jana Alhamisi alipokutana na Jamie Dimon, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na ofisa mtendaji mkuu wa JPMorgan Chase alisema, China inakaribisha kampuni zinazowekezwa na Marekani kuendeleza kwa kina siku hadi siku ushirikiano wa kunufaishana na China, na kuendelea kuchangia maendeleo mazuri, tulivu na endelevu ya uhusiano wa China na Marekani.
He amesema mazungumzo ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani yamepata maendeleo ya hali halisi, na yakiweka mazingira kwa nchi hizo mbili kuendelea na ushirikiano wao wa kiuchumi na kibiashara.
Amesema China inafanya jitihada za kujenga soko kubwa la pamoja la nchi, kuanzisha muundo mpya wa maendeleo, na itaendelea kupanua ufunguaji wake mlango wa kiwango cha juu kwa dunia.
Dimon amesifu matokeo ya mazungumzo ya kiuchumi na kibiashara kati ya Marekani na China, akisema JPMorgan Chase itaendelea kuzidisha ushiriki wake katika soko la mitaji la China, na kuhudumia vyema kampuni kubwa za kimataifa katika kufanya biashara nchini China na kampuni za China katika kujiendeleza nchi za nje.
Shughuli za kiutamaduni zafanyika kwenye Jukwaa la Russia na China mjini Khabarovsk, Russia
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma