

Lugha Nyingine
Wanachama wa WTO isipokuwa Marekani wakosoa sera ya ushuru ya Trump, na kutoa wito wa kuimarishwa kwa mfumo wa biashara wa pande nyingi
GENEVA - Umoja wa Ulaya (EU) na wanachama wengine wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) zimepinga ushuru wa forodha wa Marekani mjini Geneva, zikitoa wito wa juhudi za pamoja za kuimarisha mfumo wa biashara wa pande nyingi.
Siku ya Jumatano, ujumbe wa EU ulianzisha ajenda juu ya mgawanyiko wa biashara duniani unaosababishwa na ushuru kwenye mkutano wa Baraza Kuu, chombo cha juu cha maamuzi cha WTO.
Ujumbe huo umesisitiza kuwa nchi zote wanachama wa WTO wameathiriwa kwa kiasi kikubwa na ushuru huo wa Marekani na baadhi ya sera zisizo za uwazi za Marekani, ambazo "zinasababisha hali ya kutokuwa na uhakika kwa kiasi kikubwa katika mfumo na gharama za kiuchumi kote duniani, na kuimarisha mgawanyiko wa biashara duniani."
Ujumbe huo wa Umoja wa Ulaya umesema mbinu ya Marekani ya kushughulikia kukosekana uwiano wa uchumi wa jumla wa nchi hiyo kupitia zana za biashara za uchumi mdogo kama vile ushuru ni suluhu isiyo sahihi.
Siku hiyo hiyo, Singapore na Uswizi zilianzisha ajenda nyingine kwa niaba ya makumi ya nchi wanachama wa WTO kujadili jinsi ya kuunga mkono mfumo wa biashara wa pande nyingi unaozingatia sheria.
Zimesema katika taarifa kwamba tangu kuanzishwa kwake mwaka 1995, WTO imekuwa na jukumu muhimu katika kutoa mfumo wa biashara duniani unaotabirika, wenye uwazi, usio na ubaguzi na wa wazi. Zimetoa wito wa kuimarishwa kwa mshikamano na ushirikiano, hatua madhubuti na za pamoja, na mageuzi ya kina ya WTO ili kukabiliana na changamoto zinazokabili biashara duniani.
Ujumbe wa China nao umesema kwamba "ushuru wa kulipiza kisasi" wa Marekani umedhoofisha sana mfumo wa biashara wa pande nyingi, kuathiri uchumi wa dunia, na kudhuru maslahi ya nchi zinazoendelea na kutoa wito wa kuchukua hatua za kushughulikia ipasavyo athari za uamuzi wa upande mmoja na kujihami kibiashara kwa kulinda na kuimarisha maadili kuu na kanuni za msingi za WTO.
"Wakati huo huo, nchi wanachama wa WTO zinapaswa kushirikiana ili kuendeleza marekebisho ya muundo wa biashara duniani, kujenga upya minyororo ya uzalishaji na usambazaji iliyovurugika kupitia ufunguaji mlango na ushirikiano, na kupunguza vizuizi vya kibiashara kwa moyo wa kuheshimiana na kunufaishana," ujumbe wa China umeeleza.
Kwenye mkutano huo wa Jumatano, wawakilishi wapatao kumi, wakiwemo wale kutoka Uingereza, Canada, Australia, Japan na Brazili, walipaza sauti za ukosoaji wa hatua za ushuru za Marekani kwa niaba ya nchi wanachama zaidi ya 100 wa WTO.
Mkurugenzi Mkuu wa WTO Ngozi Okonjo-Iweala ametoa wito kwa Marekani kushiriki katika mazungumzo ya kiujenzi na pande husika.
Shughuli za kiutamaduni zafanyika kwenye Jukwaa la Russia na China mjini Khabarovsk, Russia
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma