Namibia yaidhinisha kujiunga na mfuko wa maendeleo ya kikanda wa SADC

(CRI Online) Mei 23, 2025

Waziri wa teknolojia ya habari na mawasiliano wa Namibia Bibi Emma Theofelus ametoa taarifa akisema baraza la mawaziri la Namibia limeidhinisha kusaini makubaliano ya kujiunga na mfuko wa maendeleo ya kikanda (RDF) wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Bibi Emma amesema kujiunga kwa Namibia kwenye mfuko huo kunatazamiwa kuboresha njia ya upatikanaji wa ufadhili wa maendeleo wa kikanda na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi ndani ya SADC.

Ibara ya 26A ya mkataba wa SADC inatoa fursa ya kuanzishwa kwa mfuko huo kwa lengo la kukusanya rasilimali kutoka kwa nchi wanachama, washirika wa maendeleo, na sekta binafsi kusaidia maendeleo ya kikanda na kuimarisha ushirikiano wa kikanda.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha