

Lugha Nyingine
Kenya yatoa mwito wa kuwepo kwa ufadhili jumuishi wa kilimo barani Afrika
Kenya imetoa wito wa ufadhili jumuishi zaidi na unaozingatia mazingira kwenye sekta ya kilimo barani Afrika, ili kuongeza uzalishaji wa chakula huku kukiwa na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi.
Mkuu wa Mawaziri wa Kenya na waziri anayeshughulikia mambo ya nje na diaspora wa Kenya Bw. Musalia Mudavadi, amesema mfumo wa sasa wa ufadhili hauendani na fursa kubwa iliyopo kwenye sekta ya kilimo.
Akiongea mjini Nairobi kwenye mkutano kuhusu Ufadhili Endelevu wa Mifumo ya Chakula na Kilimo, Bw. Mudavadi ametoa wito wa kuhama kutoka kwenye mbinu za mwitikio wa haraka na biashara, hadi mbinu madhubuti za kuleta mageuzi yanayoibua fursa kwenye mambo ya ardhi, nguvukazi, na ujuzi wa wenyeji ikiwa ni sehemu ya mkakati wa pamoja wa ukuaji endelevu.
Shughuli za kiutamaduni zafanyika kwenye Jukwaa la Russia na China mjini Khabarovsk, Russia
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma