

Lugha Nyingine
UN yaonya kuhusu kuzorota kwa hali ya kibinadamu nchini Sudan
Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu kuzorota kwa hali kibinadamu nchini Sudan, wakati vita vikiendelea.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric, amesema kuongezeka kwa mapigano nchini Sudan kunafanya raia kukimbia makazi yao na kwenda kwenye makazi ya hifadhi.
Amesema kuwa, katika Jimbo la Kordofan Magharibi watu elfu 47 wa miji ya Khiwai na Nuhud wamekimbia makazi yao, wengi wao tayari walikuwa wakimbizi wa ndani na sasa wamelazimika kukimbia makazi yao kwa mara ya pili.
Aidha, amesema kuwa, katika Jimbo la Darfur Kaskazini takriban watu 1,000 wamekimbia makazi yao kutoka kambi ya Abu Shouk na mji wa El Fasher, na kufanya jumla ya watu waliokimbia makazi yao kutoka maeneo hayo mawili kwa mwezi huu kufikia 6,000.
Amesema, kwa jumla, Darfur Kaskazini inakadiriwa kuwa na watu milioni 1.7 waliokimbia makazi yao.
Katika maelezo yake ameeleza kuwa, kupanda kwa bei ya chakula na kuongezeka kwa maambukizi ya kipindupindu katika baadhi ya maeneo ya Jimbo la Khartoum, pia kunachochea msukosuko.
Shughuli za kiutamaduni zafanyika kwenye Jukwaa la Russia na China mjini Khabarovsk, Russia
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma