

Lugha Nyingine
Rais Xi atuma barua ya pongezi kwa Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Eneo la Magharibi mwa China
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametuma barua ya pongezi jana Jumapili kwa Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Eneo la Magharbi mwa China, yanayofanyika Chengdu, Mkoa wa Sichuan, kusini-magharibi mwa China.
Rais Xi amesema kuwa maonyesho hayo mwaka huu yanalenga kupanua ufunguaji mlango kwenye kiwango cha juu, kuendeleza kwa kina ushirikiano wa kikanda, na kuhimiza ujenzi wa mfumo wa viwanda vya kisasa.
“Maonyesho hayo yana umuhimu kwa kuhimiza kuanzishwa kwa hali mpya ya maendeleo na ujenzi wa pamoja wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kutoa jukwaa madhubuti kwa nchi mbalimbali duniani kutumia pamoja fursa za maendeleo katika eneo la magharibi mwa China,” Rais Xi amesema.
Akisisitiza kwamba mshikamano unajenga mafanikio kwa pamoja, na ushirikiano unaweza kuleta maendeleo kwa pamoja, China inapenda kuchukua maonyesho hayo kama fursa ya kuongeza maelewano, kuimarisha urafiki, na kuzidisha ushirikiano na marafiki kutoka nchi zote.
“China itashikilia mfumo wa biashara ya pande nyingi na kuhakikisha mzunguko tulivu na rahisi wa minyororo ya kimataifa ya viwanda na usambazaji bidhaa pamoja na dunia, na kuingiza msukumo mpya katika ustawi na maendeleo ya uchumi wa dunia,” Rais Xi amebainisha. Maonyesho hayo yamefunguliwa mjini Chengdu jana Jumapili chini ya kaulimbiu ya "Zidisha Mageuzi kwa Kuongeza Msukumo, Panua Uwazi kwa Kuhimiza Ukuaji" yakiwa yameandaliwa na Serikali ya Mkoa wa Sichuan.
Shughuli za kiutamaduni zafanyika kwenye Jukwaa la Russia na China mjini Khabarovsk, Russia
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma