

Lugha Nyingine
China imejiandaa kikamilifu kwa mishtuko ya nje, Waziri Mkuu awaambia wafanyabiashara
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria kongamano la makampuni za China nchini Indonesia, mjini Jakarta, Indonesia, Mei 25, 2025. (Xinhua/Li Xiang)
JAKARTA - Waziri Mkuu wa China Li Qiang jana Jumapili wakati akihutubia kongamano la kampuni za China zinazofanya shughuli zake nchini Indonesia, ameziambia kampuni hizo kuwa China imejiandaa kikamilifu kwa mishtuko ya nje akisema tangu mwanzoni mwa mwaka huu, uchumi wa China umeendelea kuimarika na kuboreka, huku biashara ya nje hasa ikionyesha uhimilivu mkubwa.
Wawakilishi kutoka kampuni zikiwemo za China Energy Investment Corporation, Huawei, SAIC Motor, New Hope Group, Tsingshan Holding Group, na TCL Technology Group walishiriki katika kongamano hilo.
Baada ya kusikiliza maelezo kutoka kwa wawakilishi wa kampuni hizo, Waziri Mkuu Li amesema kuwa kwa sasa utaratibu wa kimataifa wa uchumi na biashara umeathiriwa sana na kwamba mgawanyiko wa minyororo ya viwanda na usambazaji umeongezeka, na vizuizi vya kibiashara vimeongezeka, ikileta athari kubwa katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi zote.
"Ikikabiliana na hatari na changamoto, China imeimarisha marekebisho ya sera ya jumla ya kukabiliana na hatari na changamoto, na imetekeleza sera ya fedha inayofanya kazi kikamilifu kabla ya athari na sera ya fedha iliyolegea kiasi," Waziri Mkuu Li amesema.
"China inaanzisha hatua husika kutuliza hali za ajira na uchumi," amesema, akiongeza kuwa nchi hiyo pia inatafiti na kuandaa zana mpya za sera, zikiwemo hatua zisizo za kawaida, ambazo zitatekelezwa mara moja katika kuitikia hali zinazobadilika.
"China ina imani na uwezo wa kuhimiza uboreshaji endelevu wa ufanisi wa uchumi," amesisitiza.
Akibainisha kuwa si rahisi kwa kampuni za China kufanya shughuli nje ya nchi, Waziri Mkuu huyo amesema China itaendelea kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na nchi nyingi zaidi, kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kampuni za China kufanya shughuli nchi za nje, na kutoa fursa na uungaji mkono zaidi, ikiwemo uungaji mkono wa kisera zaidi.
Waziri Mkuu huyo wa China ameelezea matumaini yake kwamba kampuni za China zitaendelea kujitahidi kwa ubora, kuimarisha uwepo wao thabiti nchini Indonesia na kupanua biashara zao katika Jumuiya ya nchi za Asia Kusini Mashariki.
Ametoa wito kwao kutumia kikamilifu faida zao bora ili kuchunguza masoko mapya na kuinua ubora wa maendeleo na faida zao, kusaidia bidhaa na huduma za China kupata ufikiaji bora wa masoko ya kimataifa.
Shughuli za kiutamaduni zafanyika kwenye Jukwaa la Russia na China mjini Khabarovsk, Russia
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma