

Lugha Nyingine
China yaanzisha matumizi ya roboti katika ukaguzi wa treni za uchukuzi mizigo
Roboti ya ukaguzi ikikagua treni ya uchukuzi wa mizigo kwenye karakana ya matengenezo ya treni ya Kampuni ya Vifaa vya Reli ya China Energy katika Bandari ya Huanghua, Mkoa wa Hebei, Kaskazini mwa China, Mei 15, 2025. (Picha na Zhang Shiqi/Xinhua)
Seti ya kwanza ya roboti za teknolojia za kisasa za ukaguzi wa treni za mizigo nchini China imeanza kutumika katika Bandari ya Huanghua, Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China, zikionyesha uwezo wa juu wa kukagua treni 10 kwa siku.
Wang Peng, Naibu Meneja Mkuu wa kampuni ya matengenezo ya Suning tawi la kampuni hiyo, amesema kuwa roboti hizo zimefikisha kiwango cha asilimia 100 cha utambuzi wa hitilafu ya kawaida ya treni.
“Seti hiyo ya roboti - moja ikikagua sehemu ya chini ya treni, na mbili zikikagua pande zake - zinaweza kukagua mabehewa 54 ndani ya dakika 135,” amesema Wang.
Tangu kufanya kazi kwa mara ya kwanza Mei 11, mfumo huo wa roboti za ukaguzi umetumika katika karakana ya matengenezo ya treni ya Huanghua.
Wang amesema kuwa idadi ya roboti za ukaguzi wa pande za treni inatarajiwa kufikia 10 ndani ya miezi minne. Wakati huo huo, kazi ya ukaguzi ambayo hapo awali iliwachukua watu 16 zaidi ya dakika 50 kumalizika, itakamilishwa na timu ya roboti ndani ya dakika 27 tu.
“Roboti kwa kweli hufanya kazi kwa usahihi zaidi kuliko binadamu,” amekiri Lyu Dawei, mfanyakazi mkongwe wa matengenezo ambaye hutumia vifaa maalum kupima vipimo vya magurudumu wakati wa ukaguzi wa treni.
Amesema kuwa ni kazi ngumu hasa kukagua sehemu ya chini ya treni, kwa kuwepo kimo kifupi cha sentimita chini ya 50 kutoka ardhini.
“Wakati wa ukaguzi wa bila zana wa maeneo yenye nyufa au uvujaji mafuta, nililazimika kuinama ili kupata uoni wa karibu zaidi. Baada ya kukagua mabehewa 54, miguu yangu ilikuwa ikihisi kufa ganzi,” amesema.
Huanghua, ikiwa ni bandari muhimu ya nishati kaskazini mwa China, inatarajiwa kushuhudia kuwasili kwa treni za mizigo zaidi ya 50,000 mwaka huu, hasa kwa usafirishaji makaa ya mawe.
Wafanyakazi wakitumia kishikwambi kukagua sehemu ya hitilafu iliyoripotiwa na roboti ya teknolojia ya kisasa ya ukaguzi kwenye karakana ya matengenezo ya treni ya Kampuni ya Vifaa vya Reli ya China Energy katika Bandari ya Huanghua, Mkoa wa Hebei, Kaskazini mwa China, Mei 15, 2025. (Picha na Fu Xiuzhi/Xinhua)
Roboti ya ukaguzi ikijiandaa kukagua treni ya mizigo kwenye karakana ya matengenezo ya treni ya Kampuni ya Vifaa vya Reli ya China Energy katika Bandari ya Huanghua, Mkoa wa Hebei, Kaskazini mwa China, Mei 15, 2025. (Picha na Fu Xiuzhi/Xinhua)
Shughuli za kiutamaduni zafanyika kwenye Jukwaa la Russia na China mjini Khabarovsk, Russia
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma