

Lugha Nyingine
Rais Xi azitaka China na nchi za Asia ya Kati kuhimiza ujenzi wa pamoja wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja
Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba kwenye Mkutano wa pili wa Kilele wa China na Asia ya Kati mjini Astana, Kazakhstan, Juni 17, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)
ASTANA - Rais wa China Xi Jinping kwenye hotuba yake Jumanne kwenye mkutano wa pili wa kilele wa China na nchi za Asia ya Kati ulioandaliwa na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev ametoa wito kwa China na nchi za Asia ya Kati kuhimiza ujenzi wa pamoja wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na kusonga mbele kuelekea lengo la kujenga jumuiya ya China na Asia ya Kati yenye mustakabali wa pamoja chini ya mwongozo wa Moyo wa China na Asia ya Kati.
Kwenye mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Rais wa Kyrgyzstan Sadyr Japarov, Rais wa Tajik Emomali Rahmon, Rais wa Turkmenstan Serdar Berdimuhamedov na Rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev, Rais Xi ameeleza kuwa wakati wa mkutano wao uliofanyika Xi'an miaka miwili iliyopita, kwa pamoja walielezea Dira ya Xi'an kwa ushirikiano kati ya China na Asia ya Kati.
"Miaka miwili imepita, China na nchi za Asia ya Kati zimezidisha zaidi ushirikiano halisi wa ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja," amesema, akikumbuka ushirikiano wa hali ya juu katika sekta mbalimbali.
Rais Xi ametoa wito kwa nchi hizo sita kufuata Moyo wa China na Asia ya Kati, na kuimarisha ushirikiano kwa nguvu mpya na hatua za kivitendo zaidi.
Ili kufanikisha hilo, ametoa maoni yake kama yafuatayo:
"Kwanza, China na nchi za Asia ya Kati zinapaswa kuendelea kudhamiria kwenye lengo la msingi la mshikamano, na daima kuaminiana na kuungana mkono," amesema.
Pili, China na nchi za Asia ya Kati zinapaswa kuboresha mfumokazi wa ushirikiano ili kuufanya kuwa wenye mwelekeo wa matokeo zaidi, ufanisi zaidi na ulio jumuishi kwa kina zaidi.
"Tatu, China na nchi za Asia ya Kati zinapaswa kuanzisha mfumokazi wa usalama kwa ajili ya amani, utulivu na mshikamano, kuongeza juhudi za usimamizi wa amani ya kikanda, kuzidisha ushirikiano wa usimamizi wa utekelezaji sheria na usalama, kwa pamoja kuzuia na kupinga fikra kali, na kupambana kithabiti na ugaidi, kujitenga na misimamo mikali, ili kudumisha amani na utulivu katika kanda."
"Nne, China na nchi za Asia ya Kati zinapaswa kuimarisha uhusiano wa maono ya pamoja, mapatano na kupendana kati ya watu wao," China itaongeza ushirikiano kati ya mabunge, vyama vya siasa, wanawake, vijana, vyombo vya habari na jumuiya za washauri bingwa na nchi za Asia ya Kati, kufanya mawasiliano ya kina kuhusu uzoefu wa utawala, na kuanzisha vituo zaidi vya utamaduni, matawi ya vyuo vikuu na karakana za Luban katika Asia ya Kati ili kutoa mafunzo kwa vipaji vya hali ya juu zaidi kwa nchi za Asia ya Kati.
Tano, China na nchi za Asia ya Kati zinapaswa kufuata utaratibu wa kimataifa wa haki na halali na ulio wa usawa na wenye utaratibu, zinapaswa kushirikiana pamoja kwa kutetea haki na usawa wa kimataifa, kupinga umwamba na siasa ya mabavu, na kuhimiza dunia ya ncha nyingi yenye usawa na utaratibu na utandawazi wa uchumi wenye manufaa na jumuishi kwa wote.
Tokayev na viongozi wengine wanne wa Asia ya Kati kwa kauli moja wamesema kwamba utaratibu huo wa mikutano kati ya China na Asia ya Kati umekuwa jukwaa muhimu la kuhimiza mazungumzo na ushirikiano, na pia kuendeleza maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi za Asia ya Kati.
Pande zote pia zimekubaliana kuwa China itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa tatu wa Kilele kati ya China na Asia ya Kati mwaka 2027.
Rais wa China Xi Jinping, Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev, Rais wa Kyrgyzstan Sadyr Japarov, Rais wa Tajikistan Emomali Rahmon, Rais wa Turkmenstan Serdar Berdimuhamedov na Rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev wakiwa katika picha ya pamoja mjini Astana, Kazakhstan, Juni 17, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
Rais wa China Xi Jinping akitembea kuingia kwenye ukumbi wa Mkutano wa pili wa Kilele kati ya China na Asia ya Kati mjini Astana, Kazakhstan, Juni 17, 2025. (Xinhua/Ding Lin)
Rais Xi Jinping wa China akipeana mkono na Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev mjini Astana, Kazakhstan, Juni 17, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba kwenye Mkutano wa pili wa Kilele kati ya China na Asia ya Kati mjini Astana, Kazakhstan, Juni 17, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)
Rais Xi Jinping wa China, Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev, Rais wa Kyrgyzstan Sadyr Japarov, Rais wa Tajikistan Emomali Rahmon, Rais wa Turkmenstan Serdar Berdimuhamedov na Rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev wakishuhudia uzinduzi wa kituo cha ushirikiano wa kupunguza umaskini cha China na Asia ya Kati, kituo cha mawasiliano na ushirikiano wa elimu cha China na Asia ya Kati, kituo cha ushirikiano wa kudhibiti hali ya kuenea kwa jangwa cha China na Asia ya Kati na jukwaa la ushirikiano wa kuwezesha biashara cha China na Asia ya Kati mjini Astana, Kazakhstan, Juni 17, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma