Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 09, 2025
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Wafanyakazi wakiwa na pilika nyingi katika sehemu ya ujenzi wa Daraja la Bonde Kubwa la Mto Huajiang katika Mkoa wa Guizhou, kusini-magharibi mwa China, Juni 6, 2025. (Xinhua/Yang Wenbin)

GUIYANG - Wakati wafanyakazi wakianza kuondoa kreni na kufunga lifti, ujenzi wa Daraja la Bonde Kubwa la Mto Huajiang, unatazamiwa kukamilika katika nusu ya pili ya mwaka 2025, na daraja hilo litakuwa daraja lenye urefu zaidi duniani.

Ujenzi wa daraja hilo ni mradi wa kampuni ya Kundi la Uwekezaji wa Usafirishaji la Guizhou, kimo cha daraja hilo kina urefu wa wima wa mita 625 kutoka sitaha ya daraja hadi kwenye maji ya mto.

Daraja hilo lenye urefu wa ulalo wa mita 2,890, na kuenea mita 1,420, pia ni daraja kubwa zaidi duniani kujengwa katika sehemu za milimali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha