Rais Xi wa China asema ushirikiano kati ya China na Kyrgyzstan una uwezo mkubwa

(CRI Online) Juni 18, 2025

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China, amekutana na mwenzake Rais Sadyr Japarov wa Kyrgyzstan jana Jumanne pembezoni mwa Mkutano wa Pili wa Kilele kati ya China na Asia ya Kati nchini Kazakhstan akisema kuwa ushirikiano kati ya China na Kyrgyzstan una uwezo mkubwa.

Amesema, China inapenda kushirikiana na Kyrgyzstan kuendelea kuzidisha kuwiana kwa mikakati yao ya maendeleo, na kuendelea kuungana mkono kithabiti katika maslahi ya msingi na masuala muhimu, ili kulinda maslahi ya pamoja na ya muda mrefu ya pande hizo mbili.

Kwa upande wake, Rais Japarov amesema, Kyrgyzstan inaweka umuhimu mkubwa kwenye uhusiano wake na China, na China ni mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara na uwekezaji wa Kyrgyzstan.

Amesema Kyrgyzstan inapenda kuimarisha ushirikiano wake na China katika nyanja mbalimbali zikiwemo za nishati na uendelezaji madini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha