

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Turkmenistan
(Picha/Xinhua)
Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na mwenzake wa Turkmenistan Gurbanguly Berdymuhamedov jana Jumanne na kusema kuwa China na Turkmenistan zinafurahia msingi imara wa kuaminiana kisiasa, na zina nia thabiti ya kushirikiana na nguvu bora ya kunufaishana.
Kwenye mkutano huo uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa pili wa Kilele kati ya China na Asia ya Kati unaofanyika mjini Astana, Kazakhstan, Rais Xi ameeleza kuwa China inapenda kufanya kazi na Turkmenistan kufungua kikamilifu nguvu bora za ushirikiano katika msingi wa kuheshimiana na ushirikiano wa kunufaishana.
Amesema, China iko tayari kushirikiana Turkmenistan kuongeza zaidi kina, upana na kiasi cha ushirikiano wa pande mbili na kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake Rais Berdymuhamedov amesema, anafurahia kukutana na Rais Xi pembezoni mwa mkutano huo wa kilele kati ya China na Asia ya Kati, na kwamba ana imani kuwa mkutano huo si tu utahimiza ushirikiano kati ya nchi za Asia ya Kati na China, bali pia utahimiza ushirikiano wa pande mbili kati ya Turkmenistan na China.
Amesema, kuendeleza kwa kina uhusiano wa pande mbili kuna maana muhimu ya kimkakati na kwamba Turkmenistan inapenda kupanua kwa pande zote ushirikiano na China, kuongeza mauzo ya gesi asilia kwa China, kuimarisha ushirikiano wa sekta zisizo za maliasili ikiwemo uundaji mashine, na ufumaji wa vitambaa.
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma