Rais Xi atoa wito kwa China na Uzbekistan kuanzisha hatua zaidi za uhuria na uwezeshaji biashara

(CRI Online) Juni 18, 2025

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China kwenye mazungumzo na mwenzake wa Uzbekistan Shavkat Miromonovich Mirziyoyev mjini Astana, nchini Kazakhstan pembezoni mwa Mkutano wa Pili wa Kilele kati ya China na Asia ya Kati ametoa wito kwa China na Uzbekistan kuanzisha hatua zaidi za uhuria na uwezeshaji biashara.

Rais Xi Jinping ameeleza kuwa alikutana na Rais Mirziyoyev mara mbili mwaka jana mjini Beijing na Astana ambapo wamefanya mipango ya kimkakati ya kuendeleza uhusiano kati ya China na Uzbekistan, na kwamba ushirikiano wa pande mbili umekuwa na mwelekeo wa kupanuka katika nyanja zote na kupiga hatua haraka.

Amesema, China inapenda kuimarisha uratibu wa mikakati ya maendeleo na mabadilishano ya uzoefu wa utawala wa taifa na Uzbekistan, kutekeleza miradi mingi zaidi ya ushirikiano wa kunufaishana, na kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake Rais Mirziyoyev amempongeza mwenzake Xi kwa kuweka kipaumbele kwenye maendeleo bora ya hali ya juu, na kuongoza China kupata maendeleo tele ya kijamii na kiuchumi.

Amesema, Uzbekistan inatilia maanani uhusiano wa kirafiki na China na inathamini usaidizi wa muda mrefu unaotolewa na China kwa ajili ya kuunga mkono maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Uzbekistan.

Amesema kuwa Mapendekezo Matatu ya Dunia yaliyotolewa na Rais Xi yana maana kubwa katika zama za sasa na kwamba Uzbekistan inapenda kutekeleza Mapendekezo hayo pamoja na China na kuhimiza amani na maendeleo duniani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha