Rais wa China atoa wito wa kutuliza mivutano ya Mashariki ya Kati haraka iwezekanavyo

(CRI Online) Juni 18, 2025

Rais Xi Jinping wa China amesema China ina wasiwasi juu ya kupamba moto ghafla kwa mivutano ya Mashariki ya Kati kufuatia Israel kuanzisha operesheni za kijeshi dhidi ya Iran akisema kuwa China inapinga vitendo vyovyote vinavyoharibu usalama wa mamlaka ya taifa na ukamilifu wa ardhi wa nchi nyingine.

Rais Xi ametoa kauli hiyo jana Jumanne alipokutana na Rais Shavkat Miromonovich Mirziyoyev wa Uzbekistan mjini Astan, Kazakhstan pembezoni mwa Mkutano wa Pili wa Kilele kati ya China na Asia ya Kati ambapo pamoja na mambo mengine marais hao wamebadilishana maoni kuhusu hali ya sasa ya eneo la Mashariki ya Kati.

“Mapigano ya kijeshi si majawabu ya kutatua tatizo, na kuzidishwa kwa mivutano ya kikanda hakuendani na maslahi ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa” Rais Xi amesema, akibainisha kuwa, pande zote husika zinapaswa kujitahidi kutuliza mivutano hiyo haraka iwezekanavyo ili isipambe moto zaidi.

Amesema, China inapenda kufanya juhudi pamoja na pande zote na kufanya kazi ya kiujenzi kwa ajili ya kurejesha amani na utulivu katika eneo hilo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha