Wageni 16 wapewa tuzo kwa kuhimiza ufahamu kuhusu China kupitia vitabu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 18, 2025

Hafla ya kutoa Tuzo ya 18 ya Kitabu Maalum ya China ikifanyika Beijing, mji mkuu wa China, Juni 17, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)

Hafla ya kutoa Tuzo ya 18 ya Kitabu Maalum ya China ikifanyika Beijing, mji mkuu wa China, Juni 17, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)

BEIJING - Waandishi, watafsiri na wachapishaji vitabu jumla ya 16 wa kigeni kutoka nchi 12 wametunukiwa Tuzo za Kitabu Maalum za China, heshima kubwa zaidi katika sekta ya uchapishaji vitabu ya China kwa wageni.

Wapokeaji hao, akiwemo Peter K. Bol, mwandishi wa vitabu na Charles H. Carswell Profesa katika Chuo Kikuu cha Harvard, wametunukiwa tuzo kwa mchango wao maalum wa kuhimiza mawasiliano ya kitamaduni na kufunzana kati ya China na nchi nyingine.

Kwa kutumia ufahamu wao wa kina kuhusu China, wameandika, kutafsiri, au kuchapisha vitabu kadhaa bora kuhusu nchi hiyo, vinavyoboresha mawasiliano ya kitamaduni na kutoa mchango kwa ajili ya jumuiya ya kimataifa kuifahamu China.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005, tuzo hiyo imetolewa kwa wageni 219 kutoka nchi 63. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha