

Lugha Nyingine
Iran yasema imerusha wimba jipya la droni na makombora dhidi ya Israel
Moshi ukifuka baada ya shambulizi la kombora la Iran mjini Herzliya, katikati mwa Israel, tarehe 17 Juni 2025. (Gideon Markowicz/JINI kupitia Xinhua)
TEHRAN - Shirika la habari la Iran, Tasnim limesema jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limefanya wimbi jipya la mashambulizi ya droni na makombora dhidi ya Israel jana Jumanne jioni, ikiwa ni duru ya 10 ya mashambulizi ya aina hiyo, na kikosi cha Anga cha IRGC kimerusha "makombora kadhaa ya balestiki kuelekea maeneo lengwa muhimu na ya kimkakati katika eneo linalokaliwa kimabavu.”
Mapema siku hiyohiyo ya Jumanne, Jeshi la Israel liliripoti kwamba makombora kadhaa yalirushwa kutoka Iran kuelekea Israel, na kusababisha ving'ora vya tahadhari ya mashambulizi ya anga katika maeneo mengi, ukiwemo mji wa Tel Aviv.
Jeshi hilo lilisema shambulizi hilo limepelekea mamilioni ya wakaazi katikati mwa Israeli, kando ya uwanda wa pwani, na katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu kukimbilia kwenye maeneo ya kujihifadhi.
Jeshi la Israel limesema kuwa shambulizi hilo la makombora ya balistiki, mengi yalizuiliwa kwa kunaswa. Televisheni ya Israel Chaneli 12 imeripoti kwamba mifumo ya kuzuia makombora ya THAAD ya Marekani iliyowekwa katika eneo hilo imeshiriki katika uzuiaji huo.
Shirika la uokoaji la Israel, Magen David Adom limesema hakuna majeruhi yaliyoripotiwa.
Mgogoro huo mbaya wa vita vya anga kati ya Iran na Israel umeingia siku yake ya tano, ambapo watu takriban 244 wameuawa nchini Iran na 24 nchini Israel. Kuongezeka kwa hali ya mgogoro huo kumesababishwa na mashambulizi ya kushtukiza ya Israel kote Iran siku ya Ijumaa wiki iliyopita.
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma