

Lugha Nyingine
Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani wa Majira ya Joto 2025 kufanyika mwishoni mwa Juni, Tianjin, China
Mkutano na waandishi wa habari wa Jukwaa la Uchumi Duniani la Majira ya Joto 2025 ukifanyika Beijing, mji mkuu wa China, Juni 17, 2025. (Xinhua/Xin Mengchen)
BEIJING – Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani la Majira ya Joto 2025 (2025 Summer Davos) utafanyika kuanzia Juni 24 hadi 26 katika Mji wa Tianjin, kaskazini mwa China, na maandalizi yote ya mkutano huo yamekamilika, waandaaji wamesema kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana Jumanne mjini Beijing.
Pia likijulikana kwa jina la Mkutano wa 16 wa Mwaka wa Mabingwa Wapya wa Jukwaa la Uchumi Duniani, jukwaa hilo la mwaka huu la majira ya joto la Davos litakuwa na kaulimbiu ya "Ujasiriamali katika Zama Mpya" na linatarajiwa kuwaleta pamoja washiriki 1,800 kutoka nchi na maeneo zaidi ya 90, waandaaji wameuambia mkutano huo na waandishi wa habari.
Wameeleza kuwa, jukwaa hilo la mwaka huu litafuatilia zaidi maeneo matano muhimu -- kufafanua uchumi wa dunia, mtazamo juu ya China, viwanda vinavyojitokeza, kuwekeza kwa watu na sayari ya Dunia, na nishati na nyenzo mpya.
“Kupitia mkutano huo wa mwaka huu, China itasisitiza tena dhamira yake ya kufungua mlango kwenye kiwango cha juu na kunufaika pamoja na pande nyingine duniani na fursa zinazoletwa na maendeleo ya China,” amesema Chen Shuai, ofisa wa Kamati ya Kitaifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China.
Ikiwa moja ya kanda zenye nguvu zaidi duniani, Asia inaendesha asilimia 60 ya ukuaji wa uchumi duniani, huku China ikichangia nusu yake, Gim Huay Neo, mkurugenzi mkuu wa Jukwaa la Uchumi Duniani ameeleza.
Amesema kuwa jukwaa hilo la mwaka huu litatoa fursa kwa washiriki kupata fursa ya kuelewa zaidi mwelekeo wa maendeleo nchini China na Asia.
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma