Waziri Mkuu wa China asisitiza uvumbuzi, kuongeza mahitaji ili kuhimiza ongezeko la uchumi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 19, 2025

Waziri Mkuu wa China Li Qiang, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akitembelea kampuni ya mambo ya mashine mjini Xuzhou, Mkoani Jiangsu, mashariki mwa China, Juni 16, 2025. (Xinhua/Rao Aimin)

NANJING - Waziri Mkuu wa China Li Qiang katika ziara ya ukaguzi kutoka Jumatatu hadi Jumatano katika Mkoa wa Jiangsu mashariki mwa China amehimiza juhudi za kuendeleza uvumbuzi na kupanua mahitaji yenye ufanisi ili kuhimiza uchumi kuendelea kuwa mzuri.

Katika ziara hiyo, amesisitiza juhudi za kujenga mazingira thabiti ya kuanzisha biashara na kupata mafanikio, na kuchochea uhai kwa maendeleo bora ya hali ya juu katika mchakato wa kuzidisha mageuzi na kufungua mlango.

Wakati akikagua kampuni ya mambo ya mashine mkoani humo, Waziri Mkuu Li ametoa wito wa kutumia kikamilifu teknolojia kama vile AI na nishati safi ili kuendeleza uboreshaji wa viwanda vya mashine za ujenzi kwa kulingana na wimbi la kimataifa.

“Jitihada zinapaswa kufanyika katika kuunganisha uvumbuzi na mahitaji ya viwanda, kuhimiza mafanikio mapya makubwa na uvumbuzi wa teknolojia, na kuharakisha maendeleo ya viwanda na matumizi sokoni,” Waziri Mkuu Li amesema.

Pia amesisitiza haja ya kufanya utafiti wa kina wa kimsingi, kuhimiza mafungamano mbalimbali ya taaluma na uvumbuzi, na kuimarisha ushirikiano ili kupata nafasi ongozi katika maendeleo ya sayansi na teknolojia na ya kiviwanda katika siku za usoni.

Akiwa kwenye kampuni ya mkoani humo ya vifaa vya matumizi ya nyumbani vya kutumia umeme, Waziri Mkuu Li alifahamishwa kuhusu matokeo ya mpango wa kutumia vifaa vya aina mpya badala ya vifaa vya zamani nchini humo, na akahimiza kampuni hiyo kutumia vyema sera husika ili kuibua uwezo bora wa matumizi.

Akisema kuwa soko la nchi hiyo ni kubwa na linaendelea kukua, Waziri Mkuu Li amesema kuwa China inakaribisha kampuni za kiviwanda kutoka nchi zote kuwekeza na kuanzisha biashara nchini humo.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu Li pia amesisitiza juhudi za kutumia kikamilifu mchango wa Reli ya Huduma za Uchukuzi kati ya China na Ulaya na biashara ya mtandaoni ya kuvuka mipaka ili kuimarisha mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Asia ya Kati, kupanua maeneo yao ya ushirikiano, na kuhimiza kunufaishana katika ujenzi wa pamoja wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Ssiasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akitembelea kampuni ya vifaa vya matumizi ya nyumbani vya kutumia umeme mjini Nanjing, Mkoani Jiangsu, mashariki mwa China, Juni 16, 2025. (Xinhua/Rao Aimin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha