

Lugha Nyingine
China yapanua sera ya ushuru sifuri kwa nchi zilizo nyuma kimaendeleo
GENEVA - China imeliarifu Shirika la Biashara Duniani (WTO) juu ya sera yake iliyopanuliwa ya ushuru sifuri kwa nchi zilizo nyuma kimaendeleo (LDCs) ambazo zina uhusiano wa kidiplomasia na China, ikiongeza wigo wa bidhaa kutoka asilimia 98 hadi 100.
Sera hiyo mpya, iliyoanza kutumika tarehe 1 Desemba 2024, ni sehemu ya juhudi pana za China kufungua mlango zaidi kwa nchi zilizo nyuma kimaendeleo na nchi za Afrika, ujumbe wa China umesema kwenye mkutano wa WTO mjini Geneva jana Jumatano.
Ujumbe huo pia umewaeleza wanachama wa WTO kuhusu tamko lililotolewa hivi karibuni na China na Afrika, ambapo China ilieleza nia yake ya kupanua sera yake ya ushuru sifuri kujumuisha asilimia 100 ya orodha ya bidhaa zenye kustahiki kutozwa ushuru kwa nchi zote 53 za Afrika ambazo zina uhusiano wa kidiplomasia na China.
Mbali na mpango huo wa ushuru sifuri, China iliahidi hatua zaidi za kuendeleza biashara katika bidhaa, na kuimarisha programu za mafunzo ya ujuzi na ufundi kwa nchi zilizoko nyuma kimaendeleo za Afrika.
Kwa mujibu wa ujumbe huo, hatua hizo zinalenga kujenga fursa mpya za maendeleo na msukumo wa ukuaji kwa nchi za Afrika na zile zilizoko nyuma kimaendeleo, wakati huohuo pia zikisaidia utulivu na mwelekeo mzuri wa biashara ya kimataifa.
Huku kukiwa na misukosuko inayoendelea katika biashara ya kimataifa, China imetoa wito kwa wanachama wote wa WTO kwa pamoja kudumisha utaratibu wa kimataifa wa uchumi na biashara ulio huru na wazi, na kuhimiza utandawazi jumuishi na wenye manufaa kwa wote.
Hatua hizo za China zimekaribishwa kwa wingi na wanachama wa WTO. Wawakilishi kutoka nchi zilizoko nyuma kimaendeleo, nchi za Afrika na nchi zingine wameeleza shukrani, wakisisitiza changamoto na hali ya kutokuwa na uhakika isiyo na kifani inayozikabili nchi zinazoendelea.
Wamehimiza wanachama zaidi kufuata mfano huo wa China kwa kutoa sera lengwa zenye manufaa, usaidizi wa kujenga uwezo, na uungaji mkono mwingine kwa nchi zilizoko nyuma kimaendeleo ili kusongesha mbele maendeleo jumuishi na endelevu ya biashara ya kimataifa.
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma