

Lugha Nyingine
Croatia na India zatia saini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano
Waziri Mkuu wa Croatia Andrej Plenkovic (kulia) na mwenzake wa India aliyezuru Narendra Modi wakifanya mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano wao mjini Zagreb, Croatia, Juni 18, 2025. (Josip Regovic/PIXSELL kupitia Xinhua)
ZAGREB - Waziri Mkuu wa Croatia Andrej Plenkovic amewaambia waandishi wa habari jana Jumatano baada ya kukutana na mwenzake wa India anayezuru Narendra Modi, kwamba makubaliano manne yamesainiwa ili kuimarisha ushirikiano kati ya Croatia na India.
"Makubaliano hayo yanahusisha sekta za kilimo, utamaduni na sayansi, pamoja na makubaliano ya ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Zagreb na washirika nchini India, hasa kuhusu elimu ya Indology (lugha, fasihi, utamaduni na historia ya India)" Plenkovic amesema.
Plenkovic ameeleza kuwa biashara kati ya nchi hizo mbili ilifikia thamani ya dola za Kimarekani karibu milioni 250 mwaka jana na “huu ni msingi" wa kupanua zaidi biashara kati ya pande mbili.
Modi kwa upande wake ameelezea matarajio yake ya kuhimiza uhusiano kati ya India na Croatia.
"Tutaanzisha mpango ambao si tu utatilia maanani mafunzo na mawasiliao bali pia utafuatilia viwanda vyote vya ulinzi wa nchi," Modi amesema, akiongeza kuwa pande hizo mbili pia zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta za dawa, kilimo, teknolojia ya kupashana habari, nishati mbadala na semikondakta.
Waziri Mkuu wa Croatia Andrej Plenkovic (kulia) na akisalimiana na mwenzake wa India aliyezuru Narendra Modi kwenye mkutano wao mjini Zagreb, Croatia, Juni 18, 2025. (Josip Regovic/PIXSELL kupitia Xinhua)
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma