

Lugha Nyingine
Wataalamu wakutana nchini Kenya kuhimiza usalama wa mtandao katika jumuiya ya Afrika Mashariki
Wataalamu mbalimbali wanakutana mjini Nairobi nchini Kenya kuhimiza usalama wa mtandao kwenye eneo la Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali (IGAD) katika Afrika Mashariki ili kukabiliana na matishio yanayoongezeka ya kidigitali.
Semina hiyo ya siku tatu ya mashauriano ya kikanda ambayo imeanza jana Jumatano, inajikita katika kutumia akili mnemba (AI) na usalama wa mtandao kwa ajili ya usalama, ushirikiano, na uhimilivu, na imewaleta pamoja maafisa waandamizi wa serikali na wataalam wa usalama wa mtandao kutoka nchi wanachama wa IGAD.
Akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa semina hiyo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali wa Kenya, William Kabogo, amesema matishio ya mtandao katika kanda yanaongezeka huku sekta za umma na binafsi zikizidi kukumbatia mfumo wa kidijitali.
Naye Katibu Mtendaji wa IGAD Workneh Gebeyehu ametoa wito wa kuwianishwa kwa utawala wa usalama wa mtandao, ikiwemo itifaki za kikanda za usimamizi wa utekelezaji sheria, viwango vya pamoja, na mifumo ya kukabiliana na matukio ya kuvuka mipaka.
Nejat Abdulrahman, mkuu wa Programu wa Sekta ya Usalama ya IGAD, amesema kanda hiyo inaweza kutumia ipasavyo AI kuongeza uwezo wa usalama wa mtandao ili kuhakikisha raia wanalindwa kwa hatua za usalama za tahadhari.
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma