Rais wa Tanzania azindua ujenzi wa shule 103 za ufundi stadi

(CRI Online) Juni 19, 2025

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania Jumatano amezindua rasmi mpango wa elimu wa taifa wa kujenga shule za sekondari za ufundi stadi 103 nchini humo, mradi ambao unagharimu shilingi bilioni 41.6 za Tanzania.

Rais ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mwamapalala iliyoko katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu jana Jumatano ambapo ujenzi wa shule hiyo ya mfano miongoni mwa shule hizo 103 zinazojengwa kote nchini, umeshakamilika kwa asilimia 96 na umegharimu shilingi bilioni 1.6.

Rais Samia amesema mradi huo unasisitiza ahadi ya serikali katika kutatua suala la ukosefu wa ajira kwa vijana, na kuhakikisha sekta binafsi inayozidi kukua nchini Tanzania inapata nguvu kazi yenye utaalamu wa kiufundi.

Pia amesisitiza mageuzi ya sera ya elimu nchini humo, ili kuhakikisha wanafunzi wanahitimu si tu kwa mtihani wa kitaaluma, bali wakiwa na ujuzi wa moja kwa moja wa ajira na kazi za mikono.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha