Kampuni kubwa ya biashara mtandaoni ya China JD.com yazindua huduma ya usambazaji bidhaa nchini Saudi Arabia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 19, 2025

Kifurushi cha kwanza cha bidhaa kutoka kampuni ya JINGDONG Logistics nchini Saudi Arabia kikifika mikononi mwa mkazi wa Riyadh mjini Riyadh, Saudi Arabia, tarehe 18 Juni 2025. (JD Logistics/kupitia Xinhua)

Kifurushi cha kwanza cha bidhaa kutoka kampuni ya JINGDONG Logistics nchini Saudi Arabia kikifika mikononi mwa mkazi wa Riyadh mjini Riyadh, Saudi Arabia, tarehe 18 Juni 2025. (JD Logistics/kupitia Xinhua)

RIYADH - JINGDONG Logistics, kampuni tanzu ya usafirishaji na usambazaji bidhaa ya kampuni kubwa ya biashara ya mtandaoni ya China ya JD.com, imezindua huduma ya usambazaji bidhaa kwa haraka nchini Saudi Arabia jana Jumatano, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kupanuka duniani ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo, huduma hiyo mpya, iliyopewa jina la JoyExpress, ni huduma ya usambazaji bidhaa kwa haraka ya B2C (kutoka kampuni hadi mteja) inayojiendesha yenyewe.

Ikiwa inafika katika maeneo mengi ya nchi hiyo ya kifalme, JoyExpress hutoa machaguo ya kufikisha bidhaa karibu na nyumba za watu, ikiwemo malipo ya pesa taslimu wakati wa kufikishwa bidhaa, na ufikishaji kwa haraka siku hiyo hiyo au siku inayofuata.

"JINGDONG Logistics itatoa huduma za kiwango cha juu kwa wateja wetu nchini Saudi Arabia na kuendana na mkakati wa Dira ya Saudi 2030 kwa kujikita kwake katika usafirishaji na usambazaji bidhaa na kutoa nafasi za ajira," amesema Charlie Peng, mkuu wa sehemu ya Mashariki ya Kati katika kampuni hiyo ya JINGDONG Logistics, kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo.

"Uwekezaji wa JINGDONG Logistics' nchini Saudi Arabia unaendana na dira yetu ya taifa ya kuwa kituo cha kimataifa cha usafirishaji na usambazaji bidhaa," amesema Rayan Albakri, naibu waziri wa Wizara ya Uchukuzi na Huduma za Usafirishaji na Usambazaji Bidhaa ya Saudi Arabia, kwenye hafla hiyo.

Nchini Saudi Arabia, Kampuni hiyo ya JINGDONG Logistics inajenga mtandao wa maghala, vituo vya kusafirisha na kuchambua mizigo, na idadi inayoongezeka ya vituo vya kusambaza bidhaa.

Nchini China, kampuni mama ya JD.com inaendesha maghala zaidi ya 3,600 na vituo 19,000 vya usambazaji bidhaa na utoaji huduma, ikiajiri wafanyakazi karibu 510,000 wa mstari wa mbele.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha